error: Content is protected by CRYPTO ISLAND PRO!!

KARIBU CRYPTO ISLAND PRO PLATOFORM

 

kuhusu sisi.

Karibu katika taasisi yetu ya CRYPTO ISLAND PRO hii ni taasisi ambayo itakusaidia kukuelewesha misingi muhimu tofauti ya kufanya biashara ya fursa mbali mbali zilizomo ndani ya blokchain na cryptocurrency kwenye masoko ya kimataifa moja kwa moja. Kama haufahamu chochote kuhusu cryptocurrency na blockchain au unafahamu kwa uchache tu, au unajaribu kufanya biashara (trade) haupati faida au unapata faida ndogo ndogo tu, basi tovuti hii ipo kwa ajili yako.

shape

KUHUSU CRYPTO ISLAND PRO:

Crypto island pro ni taasisi binafsi inayojishughulisha na utoaji wa mafunzo yanayohusu matumizi sahihi ya simu zetu za kiganjani juu ya fursa mbali mbali zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zinazoweza kuwa ajira kwa vijana wetu au kuwa kama nyongeza ya ajira kwa wafanya kazi (waajiriwa), wajasiriamali, na wanafunzi bila ya kuathiri ratiba zao za kila siku, kuwa badala ya kutumia simu zao kuchati au kuangalia vichekesho (comedy) muda huo wanaweza wakatumia simu zao kujitengenezea kipato cha ziada.

Taasisi hii makao makuu yake yapo ZANZIBAR. Na imeanzishwa rasmi na kusajiliwa na serikali mnamo tarehe 22/03/2022. Baada ya CEO/mkurugenzi Mr baisam kuguswa na msiba wa watu wengi nchini Tanzania na nchi jirani kupoteza fedha zao na kuibiwa na watu wasiojulikana kwa kudanganywa wawekeze pesa kwenye kampuni zao kwa kujifanya wao ni wataalamu wa biashara za mitandaoni (trade) na  watakuwa na utaratibu wa kuwalipa kila siku baada ya kuwekeza kwao, mwisho wa siku wamekimbia na pesa nyingi za wawekezaji hao.

Sasa baada ya kutokea hayo na kwa kuwa Mkurugenzi wetu MR Baisam alikuwa anazifahamu biashara hizi kwa muda mrefu na alikuwa anafaidika nazo vizuri sana yeye binafsi bila ya kuwekeza kwenye kampuni yoyote ile, Na alipo ona watu wengi sana wanaendelea kuibiwa yeye binafsi MR Baisam akaamua kuunda timu ya watu ambao wanaweza kufanya biashara hizi na kunufaika kama anavonufaika yeye, watu ambao wenye maono (idea) kwenye teknolojia mpya ya blockchain,  aliwakusanya watu hawa na kuunda timu kwa ajili ya kujifunza zaidi teknolojia hii ndani na nje ya nchi kwa wataalamu mbali mbali na hatimae wakawa na uwezo mzuri kufanya na kunufaika juu fursa hizo. Sasa kufikia tarehe 22/03/2022 wameamuwa kufungua taasisi hii kwa ajili ya kufundisha na wengine ili na wao waweze kunufaika moja kwa moja kwa mikono yao wenyewe kwenye fursa hizi bila kudanganywa na kitu chochote kile kilichopo ndani ya nchi na nje ya nchi.

CRYPTO ISLAND PRO. Malengo yetu ni kuelekea katika namna ya kuwa na weledi mpana kwa wanafunzi wetu kwenye uwanja wa fursa hizi ili waweze kujikwamua walipo na tutengeneze maisha bora kwa kila Mzanzibar, Tanzania na Afrika kwa ujumla. Hakika kwa nguvu ya pamoja tumeamua na tunaweza.

 

KWANINI UCHAGUE KUJIFUNZA NA CRYPTO ISLAND PRO?

  • Kujiunga na mafunzo yetu kutakuwezesha kuendana na dunia kupitia mapinduzi ya viwanda yanayokua kwa kasi hivi sasa kwa teknojia ya blockchain yenye fursa nyingi za uchumi wa kidigitali.
  • Taasis yetu inawakufunzi wenye uzowefu na ujuzi wa biashara wa fursa za kimtandao kwa muda mrefu na ni taasisi ya kwanza kuanzishwa hapa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla wake huku ikiwa imefuata matakwa yote ya kisheria za serikali ikiwemo usajili na ulipaji wa kodi. Kwa hakika kuwa nasi hapa basi upo katika mikono salama.
  • Taasisi yetu imejipanga vyema katika kuhakikisha unaelewa vizuri mifumo hii na unanufaika nayo moja kwa moja mifukoni mwako ili kukuwezesha kukutoa katika hali uliyopo sasa na kuelekea katika hali nyengine kimaisha.
  • Licha ya hayo pia taasisi yetu inaendelea kujipanga katika maboreshaji mbali mbali na mifumo ya kutoa vyeti (certificate) kwa wahitimu wetu baada ya kufanya mtihani na kwa wanafunzi bora kuzawadiwa zawadi nzuri mfano pikipiki, laptop, simu n.k
  • Karibu ujifunze nasi crypto island pro kwa maslahi yako binafsi na kwa watu wanaokuzunguka.

VISSION/MAONO/DIRA

01

Crypto island pro. Kuwa ni taasisi yenye ubora katika kutoa huduma zinazozingatia uaminifu pamoja kutoa mafunzo ya kitaalamu yanayohusiana na teknolojia ya blockchain na masoko ya mitandao ya fedha za kidigitali na kuhakikisha yanamnufaisha kila mdau.

MISSION/DHAMIRA

02

Kuwa na kiwango bora kinachorahisisha njia nyepesi zaidi katika kujifunza teknolojia mpya na ya kisasa ya blockchain na kufanya biashara ya fedha mtandaoni (trade) kwa urahisi katika masoko ya kimataifa na kutengeneza kipato kizuri kwa maslahi mapana kwako binafsi na watu wanaokuzunguka.

KWANINI UFANYE CRYPTO

03

  • Ni ajira ya kiganjani mwako ambayo unaweza kufanya kazi popote pale ulipo,
  • Unahitaji kiasi kidogo tu cha mtaji,
  • Haziathiriwa na mfumuko wa bei,
  • Ni fedha ambazo zinatumika duniani kote, na unaweza kufanya manunuzi online popote pale duniani.
  • Mtu yoyote anaweza kuzimiliki na kuzihifadhi bila kuingiliwa na mamlaka yoyote binafsi au ya kidola.

UONGOZI WA CRYPTO ISLAND PRO.

BOARD OF DIRECTORS. 

MR. BAISAM - FOUNDER/CEO/MKURUGENZI MTENDAJI

“inabidi tusonge mbele kwa kila hatua ili kupata mafanikio mazuri katika maisha yetu ya sasa na ya baadae, ili kuishinda khofu yako unapaswa uwe na hamasa ya kila siku. ukijihisi umechoka unataka kuacha unachokifanya basi tambua kuwa iyo ni sehemu moja wapo ya hatua katika mafanikio. CRYPTO ISLAND PRO tunaamini tunachokifanya, tunachokifanya sio kitu pekee cha kukupa maarifa tu bali pia ni kitu ambacho kinaweza kutokomeza umaskini kwako na katika nchi yako kwa ujumla”.

MR IDDI - FOUNDER/ASSISTANT DIRECTOR

“Wacha tuendelee kuwasaidia wanaohitaji msaada wa kujua kitu gani wanaweza kufanya katika kipindi hiki cha mfumuko wa bei. Wacha tuendelee kuwasaidia watu hawa wanaohitaji msaada kupitia CRYPTO ISLAND PRO ulimwenguni kote. Kama unataka kuboresha maisha yako inabidi uwe na mtazamo chanya juu ya kutafuta ujuzi na maarifa sahihi pamoja na kuyafanyia kazi maarifa hayo, hivo ndivo nilivofanya mimi kwa muda mrefu hadi sasa, na hakika ukiamua kufanya kama nilivofanya mimi basi hakika utaona dira nzuri ya muelekeo mpya wa maisha yako”

MR KHAMIS - FOUNDER/MARKETING MANAGER

“kama unahitaji mabadiliko kwako binafsi basi inakubidi ubadilike wote kuanzia tabia na hata matendo yako ili uweze kutoka hatua moja kwenda nyengine, Jambo ambalo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kufanya, watu pekee wanaoweza kufanya ni wale wanaohitaji mabadiliko ya kweli kweli, ambao wamechoka kudhalilika katika hali walizonazo kwa sasa, wanahitaji kuwa katika hali nyengine. kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawaipendi hali waliyonayo kwasasa, basi usijali kama upo serious CRYPTO ISLAND PRO ipo hapa kwa ajili ya kubadilisha maisha yako.

error: Content is protected by CRYPTO ISLAND PRO!!