Mh Raisi wa jamhuri ya muungano wa tanzania ainasihi Benki kuu ya Tanzaia (BOT). wajiweke tajari kwa kujiandaa na ujio wa teknolojia mpya ya BLOCKCHAIN na CRYPTOCURRENCY.

 

Dar es Salaam. Katika kuiandaa Tanzania kufaidika na mapinduzi ya nne ya viwanda, Rais Samia Suluhu Hassan ameigiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanza kujiandaa juu ya namna nchi itakavyotumia teknolojia ya sarafu za mtandaoni maarufu kama ‘Crypto currency’.

Wito huo wa Rais Samia ni moja ya maagizo makubwa kwa kiongozi wa juu zaidi wa Serikali katika kutazamia namna ambavyo teknolojia mpya kama ya blockchain inavyoweza kuingizwa katika mfumo rasmi wa uchumi.

Rais Samia amesema Tehama imeleta Maendeleo makubwa ulimwenguni ambapo miongoni mwa mambo hayo ni kuibuka kwa sarafu mpya zinazotumika mtandaoni za Crypto currency.

Miongoni mwa sarafu mashuhuri za mtandaoni ni Bitcoin ambayo thamani yake imekuwa ikipanda miaka ya hivi karibuni. Sarafu nyingine ni Litecoin, Cardano, Polkadot na Stellar. 

“Najua nchi nyingi duniani hazijazikubali wala kuanza kutumia sarafu hizo. Hata hivyo, wito wangu kwa benki kuu ni vyema mkaanza kufanyia kazi maendeleo hayo, kujitayarisha tu, kukaa tayari. Yakija yakitukamata, yasitukamate hatuko tayari,” amesema Rais Samia wakati akizindua jengo la BoT tawi la Kanda ya Ziwa. 

“Tunaweza tukaona sisi hatuko tayari lakini wananchi wetu wakatutangulia katika hizo ‘system’. Wakaanza kuingia huko katika nchi za nje na wakiingia huko bila shaka yatakuja huku kwetu,” ameongeza.

Mataifa mengi ulimwenguni bado yanasita kuingiza teknolojia ya blockchain na sarafu za mtandaoni katika mifumo rasmi ya kiuchumi. Sarafu za mtandaoni hutumia mfumo wa blockchain. 

Teknolojia ya blockchain ni mfumo wa tehama ambao husaidia kuweka miamala ya biashara kwa uwazi na iwapo umiliki utabadilika au kuongezeka kila mtu aliyepo kwenye mtandao huo huwa ana uwezo kung’amua kilichojiri.

Hivi karibuni El Salvador ilikuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kukubali sarafu ya mtandaoni ya Bitcoin kuwa sehemu rasmi ya sarafu katika taifa hilo inayoweza kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Leave a Comment