Seminar hii ilifanyika Zanzibar tarehe 28/08/2022. mwanakwerekwe, ukumbi wa alnoor hall.

Lengo la semina hii ni kutoa mafunzo kuhusu njia mbalimbali za kujiajiri  kupitia fursa mbaali mbali zilizopo ndani ya blockchain ambazo watu hujishughulisha nazo kwa kupitia mitandao tu ya simu ya mkononi.

WAHUSIKA WALIOHUDHURIA KATIKA SEMINAR HII NI KAMA WAFUATAO;

Mgeni rasmi; Madam Sandra Chogo.

Viongozi wa crypto island pro; Mkurugenzi Mr baisam na msadizi Mkurugenzi Mr Iddy

Wanafunzi wa crypto island pro,

Pamoja na wageni waalikwa.

  • MGENI RASMI;  Madam Sandra Chogo.
  • Blockchain profesional with marketing analysis
  • author of Jielimishe kuhusu blockchain
  • Mkurugenzi wa taasisi ya CRYPTO ISLAND PRO. MR BAISAM
  • Engineer profesional with professional trader
  • Naibu mkurugenzi wa taasisi ya CRYPTO ISLAND PRO. MR IDDY
  • financial expert with professional trader

 

Wanafunzi wa taasisi ya crypto island pro.

 

Baadhi ya wageni waalikwa

  1. Ø   Wazungumzaji.

1.     Mzungumzaji wa kwanza alikuwa ni Madam  Fatma Nassour. Yeye alisoma risala iliyohusu historia ya taasisi ya crypto island pro, changamoto zake na mafanikio  makubwa yaliyofikiwa hadi sasa.

2.       Mzungumzaji wa pili  ni Farid Hassan (mhamasishaji). Alizungumzia (Mindset) na kwa namna gani tunaweza kuyafikia mafanikio.

3.     Mzungumzaji wa tatu ni Mr Yash. Alizungumzia kwa kitaalamu kuhusu mifumo ya pembe tatu (Pyramid schemes) na vipi matapeli
wanaweza kuzitumia katika kufanya udanganyifu na nini tufanye ili tuepukane na utapeli huo.

4.      Mzungumzaji wa nne alikuwa ni MR Baisam. Alizungumzia kuhusu mapinduzi ya 4 nne ya viwanda na  changamoto zinazokuja kuleta mabadiliko ambayo hayakuwahi kuwepo duniani.

5.     Mzungumzaji wa tano alikuwa ni Madam Sabrina Sudi; aliweza kuzungumzia taasisi yao inavoweza kusaidia wafanya biashara jinsi. 

6.    Mzungumzaji wa sita ni Mr Iddi. Alizungumzia kuhusu nguvu ya internent na  kutilia mkazo  yaliyozungumzwa na wazungumzaji
waliopita.

7.    Mzungumzaji wa saba  ni mgeni rasmi Mrs Sandra J. Chogo. Alizungumzia namna gani mapinduzi ya nne ya viwanda yanavokuja kubadilisha mfumo mzima wa watu kutokana na fani zao.  Pia alizungumzia block chain Bar code, maana ya mapinduzi ya nne ya viwanda, ripoti ya tanesco, fursa katika mapinduzi ya nne ya viwanda, internent of information, internent of value (block chain), nini bitcoin, (CBDC) central Bank Digital currency ya Tanzania, tofauti kati ya block chain, crypto currency and bit coin.

 

  • Kitendo kilichofata baada ya hapo ni zoezi la maswala na majibu.
  • Zoezi la kukabidhi vyeti kwa wanafunzi bora.
  • Na zoezi la kugawa
HITIMISHO.

Kiujumla semina hii ililenga kuwahamasisha watu waweze kutambua ni wapi ulimwengu ulipo na wapi unaelekea na hatua gani wafate  ili waendane na mazingira  bila kuathiri mfumo wa maisha yetu. 

Jumla ya watu walioweza kuhudhuria katika semina walikuwa ni watu ( 300).

MAPENDEKEZO.

Iligundulika kuwa taasisi ya crypto island pro inajitahidi sana
kufundisha vizur na pia ina walimu weledi mno lakini changamoto kubwa iliyopo
kwa hii taasisi hadi sasa  ni vifaa vya
kusomeshea wanafunzi. Hivyo tunaiyomba serekali na taasisi zinazohusika na
mambo haya waweze kutoa sapoti ili taasisi hii iendelee kuwa bora Zaidi. 

 Ripoti hii imeandaliwa na ndugu RUKIA NAHODA JUMA,

                   Mwanafunzi kutoka chuo cha Fedha chwaka  Zanzibar.

HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA SHUGHULI.

 

 

SHORT VIDEO YA SHUGHULI HII HAPA CHINI.

Leave a Comment